PETR CECH ASEMA ALICHONACHO MOURINHO, WAO ARSENAL HAWANA


PETR CECH amekiri kuwa Arsenal hawana ile dhana ya kusaka ushindi kwa gharama yoyote. 

Washika bunduki wameanza msimu vibaya, wakipoteza mechi mbili kati ya tatu walizocheza. 

Lakini Cech ambaye alifanya kazi chini ya Mourinho Chelsea, amesema kocha wake wa zamani alikuwa na dhana ya kushinda kwa gharama yoyote.

Mourinho ambaye kwasasa yupo Manchester United amepeleka dhana hiyo Old Trafford ambapo klabu hiyo imeshinda mechi zake zote tatu msimu huu huku ikiwa haijaruhusu bao hata moja.

Cech amekiri kuwa ari ya 'uuaji' imekosekana kwenye kikosi cha Arsene Wenger.

Kipa huyo wa Arsenal amesema: "Wakati Mourinho alipowasili Chelsea kutoka Porto, alikuja na jambo moja kuu: ametoka katika klabu ambayo haikubali kumaliza kwenye nafasi ya pili.

"Akatuletea ari na imani ile ndani ya Chelsea. Alichofikiria ni ushindi tu, kwa gharama yoyote ile.

"Alichukia sare. Tunaporejea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na sare, tulijua wazi kuwa hataridhika".No comments