Habari

PICHA 12: KAMA SHOW YA JAHAZI YA DAR LIVE ILIKUPITA, HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA SEPTEMBA 16

on

Licha ya dosari ya kukatika umeme na onyesho kusimama kwa zaidi ya
dakika 40, lakini show ya Jahazi Modern Taarab ndani ya Dar Live Septemba 16,
ilisisimua sana.
Onyesho hilo lililopewa jina la “Usiku wa kukumbuka zamani”
liliwatendea haki mashabiki kwa asilimia 95.
Lengo la onyesho hilo ilikuwa ni kuwakumbusha mashabiki wa Jahazi
ladha za zamani kutoka kwa wasanii wao wa zamani ambao kwa sasa wanazitumikia
bendi zingine.
Wasanii wote wa zamani waliotajwa katika matangazo ya onyesho hilo,
walifika isipokuwa mmoja tu – Fatma Mcharuko wa Yah TMK – na ndio maana Saluti5
inasema Jahazi walilitendea haki onyesho hilo kwa asilimia 95.
Waimbaji kama Bi Mwanahawa Ali, Khadija Yussuf, Miriam Amour, Mwansiti
Robert na Rahma Machupa wote walikuwepo, lakini pia ilikuwepo ‘sapraiz’ ya
uwepo wa Thabit Abdul aliyetesa kwenye kinanda na magitaa yote.
Ama kwa hakika lilikuwa ni onyesho tamu lililoteka hisia za watu.
 Ally Jay akipapasa kinanda
 Amigo akiimba wimbo “Domo Kaya”
 Khadija Yussuf akiimba kwa tabasamu pana kwenye jukwaa la Jahazi
 Miriam Amour naye alikuwepo
 Mwansiti Robert akiimba wimbo “Bado Hujanuna”
 Miriam Amour akionyesha kukoshwa na Mwansiti hadi akaamua kwenda kumtunza mshiko. Mwansiti pia ndiye aliyekuwa MC wa onyesho hilo

Bi Mwanahawa Ally akiimba “Roho Mbaya Haijengi”
 Amigo akifanya vitu vyake
 Rahma Machupa akiimba “Nipe Stara”
 Thabit Abdul akikung’uta solo gitaa la Jahazi
 Bi Mwanahawa na Khadija Yussuf wakifuatilia onyesho kwa makini
Jukwaa la Jahazi lilivyonoga

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *