PICHA 20 ZA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA KHAMIS DACOTA ...ni aliyekuwa mbunge mteule wa CUF


Aliyekuwa  mteule wa ubunge wa viti maalum kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Bi Hindu Khamis Wazir Mwenda, amezikwa jijini Dar es Salaam Jumapili mchana.

Marehemu ambaye ni mama mzazi wa mtangazaji wa vipindi vya muziki wa Kiafrika kupitia Clouds FM na Clouds TV, Khamis Dacota,  amezikwa katika makaburi ya Kisutu.

Wanasiasa, wanahabari, wanamichezo na wasanii mbalimbali walikuwa sehemu ya umati uliohudhuria mazishi hayo.

Zifuatazo ni picha kadhaa za mazishi ya Bi  Hindu Khamis Wazir Mwenda.
 Marafiki wa Khamis Dacota wakiwa makaburi ya Kisutu muda mfupi kabla mwili haujawasili. Kutoka kushoto ni MC Double A, William Kaijage na Arcado Nchinga

 Mwanasiasa Idd Azan (katikati) akiwa na mtangazaji Amani Misana (kulia) wakiusubiri mwili wa marehemu 

Khalid Chokoraa (kushoto) akiwa na King Dodoo
Mwili ukiwasili makaburi ya Kisutu

Mwili wa marehemu ukipokewa na ndugu, jamaa na marafiki

Khamis Dacota (katikati) akiwasili Kisutu. Kulia ni Jose Mara
Khamis Dacota akiingia kaburini kushiriki kuhifadhi mwili wa mama yake mzazi
Jeneza likiwa limewasili kaburini

Mazishi yakiendelea

Katikati ni mwenyekiti wa CUF Prof. Lipumba
  Prof. Lipumba akishiriki mazishi
  Khamis Dacota akiwa hoi kwa kilioDescription: https://2.bp.blogspot.com/-rFS8R_3n7Iw/Waw5De6WPxI/AAAAAAAAkkQ/yzDIzPgqgGYdiBZOASBx_PAusH6Y6mYuQCLcBGAs/s1600/PICHA%2B13.jpg

 Ilikuwa siku ngumu kwa Khamis Dacota
 Ilikuwa siku ngumu kwa Khamis Dacota 

  Sehemu ya watu waliohudhuria mazishi
Wasanii Dully Sykes na Christian Bella

Dua baada ya mazishi
Watu wa karibu na marehemu wakiomba dua baada ya mazishi kukamilika
Kutoka kushoto ni William Kaijage, Rajab Zomboko wa Radio One, King Dodoo, Christian Bella na Patcho Mwamba
Khamis Dacota akifarijiwa na marafiki zake

No comments