PICHA 32: DIMBA MUSIC CONCERT ILIVYOWEKA HESHIMA JUMAMOSI USIKU JIJINI DSM


Hatimaye imebainika kuwa muziki wa dansi bado unapendwa ila kinachotakiwa ni miundo mbinu tu ya uhamasishaji sambamba na ubunifu wa mambo matamu.

Onyesho kubwa la muziki wa dansi lililopewa jina la Dimba Music Concert ambalo lilifanyika Jumamosi usiku ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel, lilifana sana.

Hakuna ubishi kuwa onyesho hilo limeleta heshima kubwa na matumaini kwa muziki wa dansi ambao uko kwenye hali mbaya sana ya kibiashara.

Ubunifu wa kuipambanisha Msondo Ngoma dhidi ya kombaini ya nyota wa dansi, ukawa chachu ya kunogesha tamasha hilo.

Umati mkubwa uliojazana Travertine Hotel, ukashuhudia namna vizazi tofauti vya dansi – wakongwe na wa kisasa – walivyoweza kutengeneza ‘remix’ ya nyimbo kali kama “Hiba”,”Wali Nazi”, “Betty”, “Jirani”, “Hadija”, “Kitambaa Cheupe” na nyingine nyingi ambazo ziliibua upya hisia za wapenda muziki.

Pata picha 32 za onyesho hilo lililoandaliwa na gazeti la Dimba linaloongoza kwa habari za michezo na burudani.
 Hassan Moshi wa Msondo Ngoma
 James Kibosho akipiga drums za kombaini ya dansi
 Karama Regeussu (kushoto) akiimba na Juma Kakere kwenye kombani ya nyota wa dansi
 Athuman Kambi wa Msondo 
 Hussein Jumbe na Karama Regessu
 James Kibosho (kushoto) na Adolph Mbinga wakifuatilia onyesho
 Kutoka kushoto ni Hussein Jumbe, King Kiki na Ally Chocky wakiimba "Kitambaa Cheupe"
 Hawa ndio waliokuwa ma-Mc wa onyesho Adam Zubeir kutoka City FM (kushoto) na Mwinyi Ami Stazo kutoka Magic FM
 Said Mabela akicharaza solo gitaa la Msondo
 Mafumu Bilal akipuliza sax ya kombaini ya dansi
 Adolph Mbinga na gitaa lake la solo
 Mtu na mtuwe ...Hussein Jumbe na wa ubani wake
 Mwinyuma Muumin jukwaani na kombaini ya dansi
 Juma Jerry ndiye aliyekuwa akipapasa kinanda cha kombaini ya dansi mwanzo mwisho
 Mashabiki wakisakata rumba
 Nyoshi el Saadat akishambulia jukwaa na Hussein Jumbe
 Nyoshi akiendelea kunogesha mambo
 Nyoshi akiimba kwa hisia kali
 Bitchuka na mbwembwe zake jukwaani
 Romario wa Msondo 
 Saad Ally Mashine kwenye drums za kombaini ya dansi
 Shukuru Majaaliwa akifukia sauti ya TX Moshi William kwenye nyimbo za Msondo Ngoma
 Kutoka kushoto ni Said Makala wa Channel Ten, Ally Chocky, Sofia Rajab wa Capital Radio na Juma Katundu
 Hassan Rehani Bitchuka mmoja wa wakali waliounda kombaini ya dansi
Mwimbaji wa zamani wa Maquis, mwanamama Tabia Mwanjelwa aliyehamishia maskiani yake barani Ulaya, naye alikuwepo Travertine Hotel
 Kutoka kushoto ni Chakuku Tumba, Juma Jerry na Hosea Bass
 Waimbaji Athuman Kambi na Twaha wa Msondo Ngoma
 Mambo yalinoga kama hivi
 Uvuruge "Smart Boy" wa Msondo na gitaa lake la kati
 Watangazaji mabingwa wa muziki wa dansi kutoka kushoto ni Masoud Masoud wa TBC, Rajab Zomboko wa Radio One na Adam Zubeir wa City FM
 Juma Katundu (kulia) akiongoza mashambulizi ya Msondo Ngoma
Rajab Zomboko wa Radio One akimpa sapoti King Kiki
Chocky na Sofia Rajab wa Capital Radio


No comments