PICHA 5: HATIMAYE DIOUF AINGIA STUDIO KUPAKUA KITU KIPYA “THE BRIDGES”


Hatimaye mwimbaji na rapa Said Msafiri maarufu kama Msafri Diouf, ameingia studio kupakua wimbo wake mpya kabisa.

Diouf ambaye kwasasa anataka ajulikane kama  Diouf Lewandowski, ameupa wimbo huo jina la “The Bridges” ambao ndani yake umejaa kilio cha mapenzi.

Wimbo huo ambao umerekodiwa katika studio za C9 Records, upo katika vionjo vya sweet reggae na umeimbwa kwa lugha mbili -  Kiswahili na Kiingereza.

Ndani ya wimbo huo utazisikia drum za Martin Kibosho na sax ya Rashid Pembe, kinanda cha C9 Kanjenje huku sauti tamu ya mwanadada Catty Chuma ikipendezesha kiitikio cha cha wimbo huo mtamu.

Diouf, msanii wa zamani wa Twanga Pepeta ambaye kwasasa anaishi Uingereza amesema atatumia likizo yake hapa nchini kutengeneza nyimbo tatu zenye mahadhi tofauti.

“Nimeanza na ‘The Bridges’ ambayo imelenga soko la ndani na nje ya nchi, baada ya hapo zitafuata zingine mbili,” alisema Diouf na kubainisha kuwa  siku chache zijazo “The Bridges” itakuwa hewani.
 Diouf kazini
  Diouf katika studio za C9
 Caty Chuma akiingiza sauti kwenye wimbo wa Diouf
 Caty akiimba kwa hisia
 Diouf na C9
Diouf na Caty baada ya kumaliza kuingiza sauti zao


No comments