PICHA 7: BOMOA BOMOA INAVYOZIDI KUNUKIA MANGO GARDEN …maduka ya Vijana Social Hall yavunjwa


Hakuna ubishi kuwa safari ya kutokomezwa kwa ukumbi wa Mango Garden Kinondoni imewadia. Tayari maduka yanayozunguka Vijana Social Hall yote yamevunjwa.

Mango Garden iko mbioni kuvunjwa ili kupisha uwekezaji mkubwa wa jengo la kitega uchumi ambalo litachukua eneo lote linalomilikiwa na Umoja wa Vijana wa CCM ikiwemo pia Vijana Hostel, Vijana Social Hall na Baobao.

Maduka yote ya kuanzia Baobao, Vijana Social Hall hadi Vijana Social Hostel yamevunjwa.

Ingawa inaaminika baadhi ya sehemu ikiwemo Vijaana Social Hall, hazitaguswa angalau kwa mwaka mmoja mbele, lakini Mango Garden na Vijana Hostel zipo kwenye sehemu ya kwanza ya mradi wa ujenzi huo mkubwa.

Ukumbi wa harusi unaopatikana nyuma ya Mango Garden nao utakwenda na maji ambapo tayari paa kubwa la eneo hilo maarufu kwa sherehe mbali mbali, limeshaezuliwa.

Mango Garden ndiyo ngome kuu ya Twanga Pepeta na Mashauzi Classic ambayo yenyewe tayari imeshasitisha maonyesho yake kwenye ukumbi huo kufuatia bomoa bomoa hiyo inayonukia kwa kasi.
Maduka yote yaliyo mbele ya Vijana Social Hall yamebomolewa
 Maduka ya Baobao nayo yamevunjwa
 Mango Garden bado iko salama, lakini muda wowote ule patabakia kuwa historia
 Ukumbi harusi wa Mango ukiwa umeshaezuliwa paa
 Ukumbi wa harusi katika sura mpya ya kukatisha tamaa
Mango Garden 'bendera' ya Twanga ikipepea huku ile ya Mashauzi ikiwa nusu mlingoti

No comments