PIUS BUSWITA AAHIDI MABAO MENGI YANGA SC


BAADA ya kutoka jela ya soka kwa kuruhusiwa kucheza Yanga, mshambuliaji Pius Buswita ametamba kuifanyia makubwa klabu yake hiyo.

Mshambuliaji huyo amesema atahakikisha analipa fadhila kwa kuifungia timu yake mabao.

Buswita amesema yuko fiti kuhakikisha anafanya kila liwezekanalo ili kuipa Yanga ushindi na hilo litawezekana kutokana na sapoti kubwa anayoipata kutoka kwa uongozi wa timu hiyo.

“Nashukuru kwa uongozi wa Yanga kunipigania hadi kupata nafasi hii ya kucheza, baada ya awali kufungiwa kwa mwaka mmoja,” amesema Buswita.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Mbao FC amesema anajutia kosa lake na kamwe hatorudia tena kwani ameshajifunza kutrokana na yaliyotokea.


Amesema, amejifunza mengi na ameuomba radhi uongozi wa TFF na klabu ambayo alitokea ya Mbao FC.


No comments