Mgogoro kati ya Edinson Cavani dhidi ya mchezaji mwenzake wa Paris Saint-Germain, Neymar unazidi kufukuta baada ya nyota huyo wa Uruguay kudaiwa kukataa ofa ya euro milioni moja ili amwachie Neymar jukumu la kupiga penalti.    

Gazeti El Pais la Hispania linadai katika mkataba wa Cavani kuna kipengele kinachohusu bakshishi (bonus) ya euro milioni 1 ambayo atalipwa mshambuliaji huyo iwapo ataibuka kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Ufaransa mwishoni mwa msimu. 

Ili kuondoa utata kati yake na Neymar, PSG ikataka kumpa mapema kiasi hicho Cavani ili akubali kuacha jukumu la penaliti kwa Neymar lakini gazeti hilo la Hispania linasema Cavani ameukataa mpango huo.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac