RASHID PEMBE KUREKODI UPYA NYIMBO ZAKE ZA VIJANA JAZZ

MKONGWE wa Saxaphone ‘Domo la Bata’, Rashid Pembe yuko mbioni kuzikusanya upya nyimbo zake zote alizotunga akiwa na bendi ya Vijana Jazz Band na kuingia Studio kuzirekodi upya, imefahamika.

Akiongea na Saluti5, Pembe amesema kuwa tayari ameanza maandilizi ya hatua hiyo iliyotokana na maombi ya mashabiki wake wengi wa ndani na nje ya nchi.

“Mashabiki wangu wamenitaka nizifanyie Remix nyimbo zangu zote za zamani nilizozifanya nikiwa na Vijana Jazz, nami katika kutii matakwa yao nimeamua kuwakubalia ili kuwaridhisha,” amesema Pembe.

Pembe amesema kuwa nyimbo hizo atazirekodi upya na kuviongezea vionjo vingi vya kisasa pamoja na miondoko ya kiasili ili kuwa na mwonekano mpya unaovutia zaidi ya ilivyokuwa awali.

No comments