RITA DOMINICK WA NOLLYWOOD AWAKUMBUKA MACHOKORAA

MWIGIZAJI wa kike nchini Nigeria, Rita Dominick amesema kuwa yupo mbioni  kuja na mipango maalum  wa kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.

Rita amesema kuwa wapo watoto wengi kwenye Taifa hilo wanahitaji msaada kutoka kwenye jamii ili waweze kupata nafasi ya kusoma, makazi bora sambamba na lishe nzuri.

"Kuna kundi kubwa la watoto wanaishi katika mazingira hatarishi bila msaada wetu wanaweza kupoteza ndoto zao," alisema staa huyo.


Kabla ya kumalizika kwa mwaka huu staa huyo atakuwa ameanza kampeni za kutunisha mfuko wake utakaolenga kuwakwamua watoto.

No comments