SAIDA KAROLI AENDELEA KUMKINGIA KIFUA MUTTA


Mkali wa muziki wa asili, Saida Karoli ameendelea kusisitiza kuwa, anavyoaminmi yeye ni kwamba Mutta amechangia kwa kiasi kikubwa kubadilisha maisha yake na kumpa umaarufu mkubwa.  

“Mengi yanaongelewa na watu kuwa eti Mutta amenufaika sana kupitia kazi zangu na kwamba mimi mwenyewe hakuna nilichokipata, lakini ukweli ni kwamba nimetoka mbali na nilipo sasa ni kwingine kabisa,” amesema Saida.


“Mutta amenisaidia sana kimafanikio na binafsi nakiri kuwa isingekuwa rahisi kwangu kufika hapa bila ya yeye. Wala hajaniibia kama wengine wanavyodai na hiki nilichokipata ndio fungu langu la haki,” aliongeza staa huyo.

No comments