SEYDON WA "SIO POA" AMUANIKA MKE WAKE MTARAJIWA

MKALI wa Bongofleva anayetamba sasa na kitu cha ‘Sio Poa’, Said Makamba ‘Seydon’ ameamua kujibu maswali ya mashabiki wake wanaohoji kuwa ataoa lini, baada ya kusema kuwa ameanza harakati za kuingia katika majukumu kama baba wa familia.

Katika mazungumzo na Saluti5, Seydon amesema kuwa yuko mbioni kukamilisha taratibu za kuachana na ukapera kwa kufunga pingu za maisha na mwanadada aliyemtaja kwa jina moja la Deborah.

“Huyu ni kati ya watu ambao wananipa sapoti kubwa isiyopimika katika sanaa yangu ya muziki, hivyo nimekata shauri kumuoana ili niweze kuwa nae karibu zaidi,” amesema Seydon ambaye pia ni mwalimu wa muziki.

Seydon amesema kuwa, tayari hatua za awali za ndoa yao zimekwishaanza na wamekushudia kumaliza biashara wakati wowote kuanzia sasa, kabla ya kuisha kwa mwaka huu.

No comments