SHABAAN YOHANA 'WANTED' ALIYETAMBA NA VIJANA JAZZ AFARIKI DUNIA BOTSWANA


MCHARAZAJI nguli wa gitaa la Solo, Shaaban Yohanna “Wanted” (Pichani) amefariki dunia jana nchini Botswana alikokuwa akifanya shughuli zake za muziki.

Mwanamuziki wa African Stars “Twanga Pepeta”, Miraji Shakashia ambaye ni mmoja wa wasanii aliyewahi kufanya naye kazi enzi zake alipokuwa Bongo, ameithibitishia Saluti5 juu ya kifo cha hicho cha Wanted.

Shakashia amesema kwamba yeye amethibitishiwa taarifa hizo na mwanamuziki Albert Chikopa ambaye anafanya shughuli zake za muziki nchini Botswana na Wanted.

“Nimewasiliana na Chikopa kupitia mtandao wa kijamii wa facebook na kunijulisha taarifa hiyo, lakini amesema taarifa zaidi atazitoa baada ya kukamilika kwa taratibu za kipolisi na uhamiaji,” amesema Shakashia.

Wanted alijipatia umaarufu mkubwa wakati akiwa Vijana Jazz alikoshiriki kurekodi nyimbo nyingi kali zikiwemo “Ogopa Tapeli”, “Ngapulila”, “Wifi Zangu, “Lumbesa”, “VIP” na “Top Queen” na nyingine nyingi.

Aliondoka nchini kati ya mwaka 1998 na 99, baada ya kupitia bendi ya Ngorongoro Heroes iliyokuwa chini ya mheshimiwa Richard Ndasa.

No comments