SHAKIRA ASEMA PENZI LAKE NA PIQUE "NDIO KWANZA LINAALIKA MAUA"


'KAPO' yenye mvuto katika ulimwengu wa soka na muziki inawahusu beki wa timu ya Barcelona, Gerrald Pique raia wa Hispania na mwimbaji Shakira ilielezwa kuwa kwenye hatari ya kuvunjika.

Katika hali ya kujibu mapigo juu ya uvumi huo wa vyombo vya habari, mrembo Shakira ameliambia jarida la HOLA la Marekani toleo la Septemba amesema penzi lao liko imara na wamejikita zaidi katika mambo ya kifamilia.

Wawili hao walianza uhusiano wa kimapenzi mwaka 2010 na tangu wakati huo wamekuwa wakionekana kuambatana pamoja maeneo yote ambayo Pique amekuwa akisafiri kwa majukumu ya kisoka.

“Tunafanya kila hali ili tuendelee kwa pamoja kwa sababu familia ndio kitu kikubwa kinachotuunganisha, tunaishi maisha yenye furaha na upendo” anaeleza Shakira.

Siku sita zilizopita, Gerrald Pique mwenye umri wa miaka 30 nae alikanusha uvumi wa kutengana na kipenzi chake Shakira mwenye umri wa miaka 40.

Uvumi wa kuvunjika kwa mahusiano ya mastaa hao, umekuja baada ya kila mmoja kutotupia picha za mwenzi wake kwenye mitandao ya kijamii tangu mwezi Juni mwaka huu.No comments