SIMBA YAWEKA MKAKATI WA KUMBADILISHA MAVUGO KISAIKOLOJIA

MSHAMBULIAJI aliyesajiliwa na Simba kwa mbwembwe nyingi, Laudit Mavugo amegeuka pasua kichwa baada ya kuwa na mwendo mbovu katika baadhi ya mechi alizocheza hivi karibuni ikiwemo dhidi ya Hard Rock ya Zanzinzibar kiasi cha kuzomewa na mashabiki uwanjani.

Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema kuwa wanahitaji kukaa kitako na mshambuliaji huyo ili kuona namna ya kunusuru kipaji chake.

"Tupo kwenye maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Azam lakini nadhani ni wakati sahihi wa kuzungumza na Mavugo ili kumuweka sawa kisaikolojia kabla ya mchezo huo,’’ alisema Mayanja.

Kinachomtokea Mavugo ni hali ya kimchezo kwa sababu yeye sio wa kwanza kupitia kipindi kigumu katika timu, lakini kikubwa ni kuona namna ya kusimama na kusonga mbele." aliongeza.


Simba inatarajia kucheza na Azam katika uwanja wa Azam Comprex jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi, mchezo ambao unatajwa kuwa na upinzani mkali kutokana na historia ya timu hizo.

No comments