SIMON MSUVA AMPA SALUTI TSHISHIMBI

KIUNGO wa timu ya Difaa Al Jadida ya nchini Morocco, Mtanzania Simon Msuva amesema kuwa tatizo la kukosekana kwa kiungo mkabaji Yanga limepata dawa kutokana na uwezo wa rasta, Papy Kabamba Tshishimbi.

Msuva ambaye aliisaidia Yanga kubeba ubingwa wa Ligi msimu uliopita amedai kwamba kwa muda mrefu kikosi hicho kilikosa mtu sahihi wa kusaidia jahazi la ulinzi.

“Nimefuatilia kwa karibu mechi za Yanga na hata zile za Simba lakini kwa kiasi kikubwa nimevutiwa na uwezo wa Tshishimbi, yule rasta nadhani ni ile shida ya muda mrefu imepata dawa sasa,” alisema Msuva.


“Binafsi bado naipa Yanga nafasi ya kuendelea kutetea taji lake baada ya kurejea kwa Ngoma na ingizo jipya la mastaa kama rasta yule, nadhani bado wana nafasi kubwa ya kufanya kitu msimu huu,” aliongeza.

No comments