"SINA JEMA" YA HALICHACHI CLASSIC YAZIDI KUWASHIKA MASHABIKI


UJIO wa kishindo wa kibao ‘Sina Jema’ cha Halichachi Classic Modern Taarab umefanya mashabiki wa mipasho kuzidi kuikubali kwa kasi bendi hiyo.

‘Sina Jema’ ni kazi mpya ya pili kwa bendi hiyo iliyo chini ya Amour Maguru ‘Chuma cha Reli’ ambayo mwimbaji wake ni Mwanahawa Chipolopolo ambaye ni mke wa bosi huyo mpapasa kinanda mahiri wa taarab.

Baadhi ya mashabiki waliozungumza na ripota wetu kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam wiki hii, wamekiri kukolezwa vilivyo na kibao hicho kilichoko kwenye miondoko inayochezeka zaidi.


“Binafsi, nimetokea kuuelewa wimbo ‘Sina Jema’ wa Halichachi Classic, hasa kutokana na mashairi yake pamoja na midundo iliyomo, nafikiri siko peke yangu, mashabiki wengi tumepagawishwa,” amesema shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Yunus Afidh.

No comments