STAA WA NOLLYWOOD KUCHEZA FILAMU YA UTUPU KWA NAILA MIL 500

MCHEZA filamu wa Nigeria, Enyinna Mwigwe amesema kuwa hakuna kitu anachohofia anaposimama mbele ya kamera, hata akitakiwa kuigiza akiwa mtupu inawezekana ikiwa tu atapewa kitita kikubwa cha fedha.

Enyinna amesema kuwa kama itatokea anahitajika kucheza sehemu zitakazomwonyesha maungo yote ya mwili wake atakuwa tayari ikiwa atapewa naila mil 500.

“Kwanini niogope kuvua nguo kwa fedha ambayo inaweza kubadilisha maisha yangu kwa muda mfupi?”

“Sanaa ni kazi yangu, sijawahi kujiuliza mara mbili ninapopewa eneo lolote kuigiza hata kama lina ugumu kiasigani,” alisema staa huyo.

Staa huyo mbali na uigizaji pia amekuwa maarufu kutokana na kazi bora ya uzalishaji ambayo anaifanya kwa muda mrefu.  

No comments