SURE BOY AZITAKA KLABU ZISIIHOFIE SIMBA SC

KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Salum Abubakar “Sure Boy” amezitaka timu ambazo bado hazijacheza na Simba, zisiihofie kwani ni timu ya kawaida sana kama zilivyo timu nyingine na kama zitakaza zinaweza kupata ushindi kwa sababu ni timu ambayo inategemea baadhi ya wachezaji tu.

Sure Boy amesema kuwa hata wao, Azam, awali walikuwa na hofu kutokana na ukubwa wa majina ya wachezaji hao lakini baada ya kumaliza dakika 45 za kwanza waligundua kuwa ni timu ya kawaida na wanaweza kupambana nayo na kupata ushindi.

“Mimi niziambie tu timu nyingine ambazo bado hazijacheza na Simba, zisihofie kwani ni timu ya kawaida sana kama ilivyo timu nyingine na kama zitakaza zinaweza kupata ushindi kwa sababu ni timu ambayo inategemea baadhi ya wachezaji,” amesema Sure Boy.

Simba inatajwa kutumia jumla ya sh. bil 1.3 katika usajili wake wa msimu huu na kupelekea kuwa kikosi ghali zaidi kikiwa na mastaa mbalimbali akiwemo Emmanuel Okwi, John Bocco na Haruna Niyonzima.

No comments