TALENT BAND YAINGIA KAMBINI KUPIKA ALBAMU YA TANO

BOSI wa Talent Band, Hussein Jumbe “Mzee wa Dodo” ameingia kambini na vijana wake kwa ajili ya kutayarisha albamu mpya wanayotarajia kuifyatua baadaye mwaka huu.

Hiii itakuwa ni albamu ya tano ya bendi hiyo inayokusanya wasanii mahiri kama vile Fadhili Musafi, Saad Ally na Babu Dallu.

Miongoni mwa kumbi ambazo Talent Band inapiga shoo na kukubalika vilivyo kwa wapenzi ni pamoja na Kisuma Mwembeyanga wanapotumbuiza mara mbili kwa wiki katika siku za Ijumaa na Jumapili.


No comments