TAREHE YA KUFUNGA DIRISHA LA USAJILI ENGLAND YABADILISHWA ...Manchester United, Manchester City 'imekula' kwao

Klabu za Ligi Kuu ya England zimepiga kura na kuidhinisha soko la kuhama wachezaji lifungwe kabla ya msimu kuanza mwaka ujao.
Hatua ya klabu hiyo za Premier League ina maana kwamba ingawa klabu zitaweza kuendelea kuuza wachezaji hadi siku hiyo, ununuzi utafikia kikomo tarehe 9 Agosti msimu wa 2018-19.
Dirisha la kuhama wachezaji kote Ulaya huendelea kuwa wazi hadi tarehe 31 Agosti na hivyo klabu zingine za Ulaya bado zitaweza kununua na kuuza wachezaji hadi hiyo 31 Agosti.
Msemaji mmoja wa moja ya vilabu hivyo, ameshutumu uamuzi huo na kusema utawapa faida wapinzani wao hususan wa Hispania ambao watakuwa na faida kuendelea na biashara ya kununua wachezaji kwa zaidi ya wiki tatu.
Vilabu vitano - Manchester United, Manchester City, Crystal Palace, Swansea na Watford - vilipinga uamuzi huo lakini kura zao hazikutosha.
Mawakala wa wachezaji wametahadharisha kuwa uamuzi huo utapandisha bei za kununua wachezaji kwa vilabu vya England kwa vile vitalazimika kumaliza biashara mapema.


No comments