Habari

THIERRY HENRY ASEMA AGUERO NDIYO MPANGO MZIMA

on

Ligu Kuu ya England kwa sasa imejaa mchuano wa washambuliaji mafundi wakiwemo Harry Kane, Alvaro Morata na Romelu Lukaku.
Hata hivyo nyota wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry, anaamini ligi hiyo ina mshambuliaji mmoja tu wa kiwango cha ‘world class’ – naye si mwingine bali ni Sergio Aguero.
Thierry Henry anasema: “Mshambuliaji pekee wa kiwango cha kidunia ni Sergio Aguero, ana weza kuibeba timu, anaweza kuichezea timu yoyote kubwa duniani na kuipa matokeo.
“Amedhihirisha hili kwa miaka mingi, kiwango chake hakijawahi kufifia, ameshinda mataji hapa. Tunastahili kumpa heshima yake.” 
Aguero tayari ameshaifungia Manchester City mabao sita msimu huu katika Premier League na laiti kama angekuwa mchoyo wa kuwatengenezea wenzake nafasi za kufunga, basi angekuwa na idadi kubwa zaidi ya magoli.
Zaidi ya mara mbili Aguero amewaduwaza wachambuzi wa soka pale alipokuwa  kwenye nafasi nzuri ya kufunga halafu badala ya kukwamisha mpira wavuni, akatoa pasi kwa wenzake ambao bila ajizi wakafunga kirahisi.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *