TONTO DIKEH WA NIGERIA ASAKA MWANAUME MWAMINIFU WA KUFUNGA NAE NDOA

TONTO Dikeh ambaye ndoa yake na aliyekuwa mpenzi wake, Olakunle Churchill, imesambaratika kama kimbunga amesema kuwa anavutiwa kufunga pingu za maiosha na mwanaume mwingine atakayekuwa mwaminifu.

Staa huyo aliyejiengua kwa muda katika ulingo wa filamu kufuatia matatizo ya ndoa yake, hivi sasa amerejea upya kazini akiwa yuko njiani kuachia filamu nyingine.

“Ninatamani tena ndoa lakini nahitaji mwanaume atakayeonyesha uaminifu na kunijali, sihitaji tena kuumizwa na mambo ya mapenzi,” alisema staa huyo.

“Nimebadili kabisa mfumo wangu wa maisha na nimekuwa nikitumia muda mwingi katika masuala ya Injili,” aliongeza.

“Nimeokoka, nahitaji kuishi maisha matakatifu. Nimebadili mienendo yangu kwa kiasi kikubwa sana,” alimaliza.

No comments