TOTO TUNDU AIFANYIA KITU MBAYA KIBAHA CARNIVAL BAND… azoa wanamuziki wote na kutambaa nao

ALIYEKUWA kiongozi mwandamizi wa Kibaha Carnival Band, Mhina Panduka “Toto Tundu” ametimka kwenye bendi hiyo na kuhamishia mabegi River Musica Band ambayo maskani yake yapo Kibaha kwa Mathias.

River Musica ni bendi mpya kabisa ambayo imeanzishwa na wanamuziki wote waliokuwa wakiunda kundi la Kibaha Carnival ambao wameachana na bendi hiyo baada ya mkataba wao kumalizika, huku sababu kubwa ikidaiwa kuwa ni maslahi.

Baadhi ya wanamuziki wengine aliosepa nao Toto Tundu ni pamoja na waimbaji; Idd Moro, Luanda Chante, Nashna Razack, Papaa Lecky ambao ni waimbaji pamoja na wapiga ala Jhonico Mafuta, Awadhi Muhumba, Elias Bass, Chacha Tumba, Awadh Kiduku na Raymond Lulandala.


Tayari River Musica Band inayomilikiwa na mfanyabiashara anayefahamika zaidi kwa jina moja la “Kinabo”, imeshaanza shoo zake ndani ya ukumbi wao wa nyumbani wa River Road Bar & Night Club ulioko Kibaha kwa Mathias, kuanzia Alhamisi hadi Jumapili kila wiki.

No comments