KIUNGO mpya wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi amesema kwamba haoni sababu ya mashabiki wa Yanga kuhofia kasi ya  watani wao Simba kwa kwani kikosi chao cha wana Jangwani kina ubora wa kutosha kutetea taji lao la Ligi Kuu msimu huu.

Katika mahojiano maalum na Saluti5, Tshishimbi amesema Simba haina kitu kikubwa kinachowatisha kama ambavyo wengi wanavyodhani na kwamba kikosi hicho cha wekundu hao kinafungika kirahisi.

"Mim sijaona kama Simba ni tishio sana labda timu zingine ambazo sijazijua lakini nilipokutana nao niliona kabisa kwamba hawana kitu kigumu kama ambavyo watu wanasema, sidhani kama wanaweza kutufanya tukose kuchukua ubingwa,’’ alisema Tshishimbi.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac