TWANGA PEPETA WAINGIA STUDIO KUFANYA ‘REMIX’ YA WIMBO WAO WA MWAKA 2001


Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta” imejitosa studio kuurudia wimbo wao “Umbeya Hauna Posho” wa mwaka 2001.

Wimbo huo unapatikana katika albam ya “Fainali Uzeeni” na sasa Twanga wameamua kuurudia na kuweka vionjo vipya pamoja na kuongeza ujumbe unaoendana na soko la sasa.

Studio iliyotumika kuurudia wimbo huo utunzi wake Ally Chocky, ni C9 Records ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

No comments