'UNADHANI WEWE NI MESSI?': NDIVYO CAVANI ALIVYOMPOKEA NEYMAR


Kumbe mambo yalianza zamani! Inaripotiwa kuwa Edinson Cavani alimuuliza Neymar kama anadhani yeye ni Lionel Messi wakati nyota huyo wa Brazil alipongia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vya PSG kwa mara ya kwanza. 

Kwa mujibu wa gazeti la El Pais la Hispania, Cavani alimuuliza Neymar kwa kusema: "Ni nani huyu? Unadhani wewe ni Lionel Messi?

Bila kujali iwapo Cavani alikuwa anakejeli au anafanya mzaha, ni wazi kuwa Neymar ambaye aliondoka Barcelona kukimbia kivuli cha Messi, hakuipokea vizuri kauli hiyo. 

No comments