VICTORIA SOUND YAPANIA KULITEKA ZAIDI SOKO LA MUZIKI WA DANSI

VICTORIA Sound ‘Wana Chukuchuku Style’ wamepania kuliteka zaidi soko la muziki wa dansi kwa kuhakikisha wanaangusha kazi kali zitakazobamba zaidi kwa mashabiki kote nchini.

Jonas Mnembuka ambaye ni Kiongozi Mwandamizi wa bendi hiyo, amesema kuwa kwa kuzingatia ushindani wa tasnia yao hivi sasa, hawana budi kufanya kitu ambacho kitawashitua wengi.

“Lazima tuhakikishe kuwa tunawavuta zaidi mashabiki wetu na katika hilo, tumeanza mkakati kabambe wa kuachia kazi zenye ubora wa hali ya juu ambazo tuna hakika zitakuwa funika bovu,” amesema Mnembuka.

Victoria Sound ni kati ya bendi kadhaa kongwe za dansi ambazo hadi leo zinaendelea kufanya vyema, hasa kwa kuwa inakusanya wanamuziki wengi wenye uwezo wa hali ya juu.

No comments