WACHEZAJI SIMBA SC WASEMA "HATUNA WASIWASI NA AZAM JUMAMOSI"

SIMBA wanatarajiwa kuwa  wageni wa Azam kwenye pambano la Ligi kuu ambalo litapigwa Jumamosi hii katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa Simba wameyapokea madiliko ya ratiba ya Ligi Kuu ambapo sasa Simba wanacheza na Azam FC kwenye dimba hilo la Azam copmplex na wameahidi kuvuna pointi tatu.

Tofauti na hisia za washabiki wengi wa soka kwamba mechi hiyo itakuwa ngumu kwa Simba kwasababu inachezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Azam, wachezaji wa wekundu hao wamesema hawana presha.

Juzi beki wa kushoto na nahodha msaidizi wa kikosi hicho, Mohammed Hussein "Tshabalala’’ amekaririwa akisema kuwa mchezo wao dhidi ya Azam utakuwa mwepesi kwao kuibuka na pointi tatu kutokana na malengo ya kupata pointi mbele ya timu yoyote ile walivyojiwekea.

Tshabalala amesema kuwa licha ya kutambua ugumu waliokuwa nao Azam lakini jambo hilo haliwazuii wao kuibuka na pointi kama ambavyo wamepania kufanya hivyo kwenye kila mchezo wao ambao watacheza msimu huu.

"Azam wagumu kwa wengine lakini kwetu watalainika tu kwa sababu hii sio mara ya kwanza tunakutana nao na tunawajua vizuri jinsi ambavyo wamekuwa wakicheza, kwamba tutumie mbinu gani kupata pointi na kizuri zaidi ni kwamba tumekusanya nyota wao ambao walikuwa tishio kwetu kwenye misimu kadhaa nyuma."

No comments