Wachezaji wa Barcelona walivaa fulana za kumpa moyo mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Ousmane Dembele ambaye ameuamia na atakosekana uwanjani kwa miezi mitatu na nusu.

Katika mchezo wa ushindi dhidi ya Eibar, wachezaji wa Barcelona wakafanya mazoezi ya kupasha mwili moto wakiwa wametinga fulana hizo za kumpa ujasiri Dembele na baadaye kupiga nazo picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza.

Dembele aliyejiunga na Barcelona msimu huu kwa pauni 96.8 akitokea Borussia Dortmund, aliumia msuli katika mchezo dhidi ya Gatafe wikiendi iliyopita.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac