WATOTO WA BOB MARLEY BADO WAKOMAA NA REGGAE LAO


DAMIAN "Junior Gong’ Marley" ameonyesha kufurahia kufanya kazi na kaka yake katika albam yake mpya ya "Stony Hill" ambayo ameshirikiana  na Stephany Marley mtoto wa tatu wa Bob Marley ambaye alizaa na Rita Marley, mke wake wa ndoa.

Stephan Marley mwenye miaka 45, amesema kwamba mara nyingi wakifanya kazi kama familia huwa inapokelewa kwa nguvu na mashabiki wa miondoko ya Reggae duniani.

“Steve amenipa nguvu katika albamu hii, huwa inafurahisha kidogo kufanya kazi kama familia, ndani yetu kuna upendo wa kipekee na mshikamano," alisema Damian (pichani juu).

“Albamu hii ina ukomavu na nyimbo nyingi zinazochezeka kama ilwe ya Welcome to Jamrok,” aliongeza.

No comments