WAZIRI SONYO NUSURA APOTEZE JICHO


Mwimbaji Waziri Sonyo anayedaiwa kumchoma kisu mwimbaji mwenzake Rama Igwe, nusura apoteze jicho katika ugomvi huo.

Tukio hilo lililotokea mjini Arusha wiki iliyopita ambapo kupitia mtafaruku baina ya waimbaji hao wawili kupitia, ikadaiwa Sonyo alimchoma kisu mwenzake na kumjeruhi vibaya.

Hata hivyo wakati Rama Igwe akisema alichomwa kisu, Sonyo amesema sio kisu bali ni chupa na kwamba alikuwa akijibu mashambulizi ya Rama.

“Rama alinikimbiza hadi kwenye bustani na kunirushia chupa ikanijeruhi jichoni na mimi nikaishika chupa ile ile na kumpelekea nayo kujibu mashambulizi,” alisema Sonyo katika mahojiano yake na TK FM.

Na sasa Waziri Sonyo ameibuka kupitia ukurusa wake wa facebook na kuweka picha yake inayoonyesha namna alivyojeruhiwa jicho lake katika ugomvi huo.

Sonyo akaisindikiza picha hiyo na maneno yafuatayo: “Sikutaka kuingia sna kwenye mitandao kwanza napata tiba ya jicho langu ndio maana nilikaa kimya maana nilimuacha aongee anavyo ongea baada isingekuwa umaahiri wangu wakukwepa chupa ningekuwa kipofu”.

Waziri Sonyo kupitia ukurusa wake wa facebook No comments