WENGER ACHEKELEA DIRISHA LA USAJILI ENGLAND KUFUNGWA MAPEMA

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amechekelea mabadiliko yaliyopitishwa na vilabu vya Premier League kubadili tarehe ya kufunga dirisha la usajili.
Kuanzia msimu ujao, dirisha la usajili England litafungwa tarehe, 9 mwezi Agosti kabla msimu mpya haujaanza tofauti na ilivyokuwa likifungwa Agosti 31.
Kocha huyo anasema: "Mambo mengi hufanyika sekunde za mwisho ambayo huwa nayajutia. Hii ndiyo maana ninaamini kwamba wakati umefika tubadilishe sheria na tuwe tukifunga soko kabla ya msimu kuanza.
"Wachezaji hawajui hatima yao. Wako ndani au nje? Kuna wengine ambao wanachukuliwa na watu alasiri ya mechi, hii ilikuwa inaumiza sana. Huwezi kuwa na wachezaji wanajiandaa kucheza huku kiakili wako nusu ndani na nusu nje."

No comments