YANGA SASA YAPATA "TIBA" YA MABAO UWANJANI

YANGA imecheza mechi kadhaa na kuonekana kama haina Fowadi mkali wa kupachika mabao, tangu kuanza kwa msimu huu.

Wana Janwani hao wameanza Ligi kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii kwa kupachika bao moja tu, huku timu ikionekana kuhangaika sana kupata mabao bila mafanikio.

Wataalam wanadai kuwa tangu kuondoka kwa Sivon Msuva na kukosekana kwa mastraika wawili, Hamisi Tambwe na Obrey Chirwa, ile kombinesheni hatari ya mabao ni kama vile imeondoka ingawa timu hiyo inaonekana kutibu idara ya kiungo.

Ukitazama kwa haraka utaona straika wa Yanga, Donald Ngoma ni mzito na ambaye hana madhara kama ilivyokuwa zamani, lakini mabeki wa timu pinzani wanamwandama wakidhani ndiye hatari zaidi.

Pia mabeki wamekuwa wakimfuata zaidi kiungo mshambuliaji mpya Ibrahimu Hajib ambaye ni fundi wa mpira, lakini kumbe wanakuwa wamejichanganya kwani nguvu ya washambuliaji wengine; Tambwe na Chirwa imekuwa imebaki nje ya uwanja.

Ngoma alisema anapocheza na wawili hao na hasa Chirwa ambaye ana kasi kama alivyo yeye, wanaifanya safu ya ushambuliaji kuamka na kuwachosha mabeki kitendo kila wakati hivyo kumpa mtu kama Tambwe uraisi wa kufunga.

‘’Ninapocheza na Chirwa ambaye ana kasi ya kupanda kama mimi inaisaidia timu kwasababu tunawachosha mabeki wa timu pinzani wanapomkaba huyu mwingine anawasumbua kwa hali hiyo pia tunafanya straika tunayecheza naye apate nafasi ya kufunga kwa urahisi."

Ngoma alitolea mfano wa mechi ya msimu uliopita dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Taifa na kusema: "Uliona mfano kwenye mechi yetu na Kagera Sugar msimu uliopita tulifunga mabao 6-2, ilikuwa na timu nzuri na ndiyo maana tulipata mabao mengi kwa sababu mtindo wetu na Chirwa uliendana."

Wakati Ngoma alisema hivyo, msemaji wa timu hiyo Dismas Ten alisema jana kuwa ana uhakika kuwa mastraika wawili wa timu hiyo Chirwa na Tambwe watakuwa wamepona tayari kucheza mechi ijayo dhidi ya Njombe Mji.

Tambew Chirwa pamoja na Goefrey Mwashuya na kipa Beno Kakolanya, wameanza mazoezi na Watanzania na kuonekana mechi zijazo.

Hali zao zinaendelea vizuri na Watanzania kurejea kutumikia timu katika mechi zijazo,’’ alisema.


‘’Kuhusiana na suala la Buswita, hili linashugulikiwa baada ya muda litapatiwa ufumbuzi,’’ aliongea.

No comments