YANGA YAILAMBA NJOMBE MJI LAKINI ULIMI NJE …Ajibu afunga bao la ‘kideoni’


Yanga SC imevuna pointi tatu muhimu baada ya kuichapa Njombe Mji 1-0 katika mchezo mgumu wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Katika mchezo huo uliochezwa mjini Njombe kwenye uwanja wa Sabasaba, alikuwa ni mshambuliaji mpya wa Yanga Ibrahim Ajibu aliyefunga bao hilo la pekee.

Ajibu alikwamisha bao tamu kwa njia ya free-kick kunako dakika ya 16 na hakuna shaka kuwa litakuwa moja ya magoli bora ya msimu huu.

Pamoja na ushindi huo, Yanga ilizidiwa sana kipindi cha pili na ni umakini tu wa kipa Youthe Rostand ndiyo ulioinyima Njombe Mji angalau bao la kusawazisha.

Njombe Mji walikitumia kipindi cha kwanza kwa kucheza rafu nyingi pamoja na soka la butua butua, lakini kipindi cha pili wakarejea kivingine na kutandaza soka la hali ya juu na kusukuma mashambulizi mengi kwenye lango la Yanga.

No comments