ZANZIBAR STARS YAZIDI KUIPASUA DDC KARIAKOO

BENDI ya Zanzibar Stars Modern Taarab ambayo imerejea kwa kishindo kwenye anga la muziki wa dansi, imeonekana kuzidi kukubalika kwa kasi kutokana na mashabiki kufuria kwa wingi ndani ya DDC Kariakoo wanakotumbuiza kila Jumanne.

Saluti5 iliyohudhuria shoo za bendi hiyo tangu kurejea kwake upya, imeshuhudia namna wapenzi wanavyoshindwa kubaki vitini wakati vibao vyao vikitumbuizwa na kujikukuta wakijimwaga katikati kucheza.

Aidha, mashabiki na wapenzi wengine wanaoonekana kunogewa zaidi hushindwa kuvumilia na kupanda jukwaani kuwatuza wasanii wanaowavutia zaidi na kufanya shoo hiyo kuonekana kuwa ni yenye mashamsham ya aina yake.


Bosi wa Zanzibar Stars, Juma Mbizo amesema kuwa hivi sasa wanatazama namna ya kuiboresha zaidi shoo yao hiyo kwa kuongeza burudani, ikiwa ni pamoja na kutoa mialiko mbalimbali kila wiki kwa wasanii wengine tofauti kumwaga burudani.

No comments