AC MILAN YAMTAKA ANTONIO CONTE MSIMU UJAO


ANTONIO CONTE anaweza akaitosa Chelsea msimu ujao na kujiunga na AC Milan ya Italia.
Wiki iliyopita kocha huyo wa Chelsea akiri kuwa ameanza kukumbuka maisha ya nyumbani kwao Italia na kusema kuwa muda si mrefu atarudi kufundisha soka Serie A.
AC Milan inataka kutumia mwanya huo kumshawishi Conte akachukue nafasi ya kocha wa sasa  Vincenzo Montella ambaye mambo hayamwendei vizuri licha kufanya usajili wa bei mbaya.

No comments