AGUERO AITAKA MAN CITY "KUACHANA" NA LIONEL MESSI

MSHAMBULIAJI wa timu ya Manchester City, Kun Aguero ameitaka klabu yake kufuta mpango wa kuwania saini ya staa wa Barcelona, Lionel Messi.

Aguero amesema kuwa klabu ya Man City inauwezo wa kifedha lakini haiwezi kupata huduma ya Messi kwani hajapanga kuondoka Nou Camp.


Man City imekuwa ikifuatilia mwenendo wa Messi ili kuona uwezekano wa kumsajili lakini wamekuwa wakikumbana na majibu ya kukatisha tamaa.

No comments