AJIBU AMTESA NIYONZIMA MARA TATU UWANJANI

KIUNGO wa Simba, Haruna Niyonzima ameonekana kuteswa na rekodi ya mshabuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib akizidiwa mambo mawili makuu.

Wakati wawili hao wakipishana kila mmoja akihamia katika klabu pinzani, Ajib usajili wake umeshaanza kulipa kwa aina tatu tofauti huku Niyonzima akiwa hana kitu.

Hali hiyo ni kwamba tangu atue Yanga, Ajib ameshaifungia timu yake mabao manne katika hatua mbili tofauti, rekodi ambayo Niyonzima ameshindwa hata kufunga bao la kuotea.

Ajib amefunga Yanga mabao mawili katika mechi za kirafiki lakini pia akafunga mabao mawili katika mechi za Ligi na kufanya afikishe jumla ya mabao manne.

Mpaka sasa Niyonzima hajafanikiwa hata kutoa pasi ya bao akiwa na Simba huku akikosa hata bao la kuotea licha ya kucheza mechi za Ligi na hata kirafiki.


Mbali na rekodi hiyo, Ajib amempiga bao lingine Niyonzima baada ya kurudishwa kikosi cha timu ya taifa ambapo juzi alishuka uwanjani wakati Taifa Stars ilipovaana na Malawi huku Niyonzima akipoteza nafasi yake katika kkosi cha Amavubi.

No comments