ALI KIBA AKUMBUKA UMUHIMU WA ELIMU

MKALI wa ngoma “Seduce Me”, Ali Kiba amezungumzia umuhimu wa msanii kuwa na elimu.

“Unajua ubongo wako ukiwa active utaweza kufikiria vitu vya msingi zaidi, achana na watu wanaoimba ujinga ni kwa sababu tu ya talent lakini elimu ni ya muhimu sana kwenye kila kitu,” amesema Ali Kiba.

Katika mahojiano ya hivi karibuni, ameeleza kuwa msanii akiwa na elimu ataweza kufikiri kwa undani zaidi na kumfanya yule anayemsikiliza kutambua msanii husika ni wa namna gani.


“Ukiwa na elimu kama wewe ni msanii ni rahisi kuonyesha watu ubongo wako ukoje kwa sababu mkasa na visa vipo na maneno yapo lakini utamfanya mtu afikirie huyu alifikiria nini,” alisema.

No comments