ALLY CHOCKY AANZISHA BENDI YAKE YA NDONDO …ni kombaini ya Twanga na Extra Bongo


Mwanamuziki mwandamizi wa Twanga Pepeta, Ally Chocky ameanzisha bendi yake ambayo itakuwa inafanya kazi katika zile siku ambazo Twanga haina maonyesho.

Bendi hiyo ambayo inajulikana kama Mwafrika, jana usiku ilitumbuiza katika ukumbi wa DDC Kariakoo kwa kiingilio kinywaji.

Wasanii wengi walioshiriki onyesho hilo ni wale waliowahi kufanya kazi na Ally Chocky katika bendi za Extra Bongo na Twanga Pepeta.

Miongoni mwa wasanii waliokuwepo DDC Kariakoo ni pamoja na Athanas Montanabe, Kabatano, Redock Mauzo, Ferguson, Hosea Bass, James Kibosho, Thabit Abdul, Miraji Shakashia pamoja na madansa kibao wa Twanga.

Hata nyimbo nyingi zilizopigwa katika onyesho hilo, zilikuwa ni za Twanga Pepeta na Extra Bongo.

Kwa mujibu wa tangazo lililokuwepo ukumbini, ni kwamba kundi hilo la Ally Chocky litakuwa likipatikana DDC Kariakoo kila Jumatano.


No comments