ALLY CHOCKY AFAFANUA KUHUSU ‘BENDI’ YAKE MPYA


Mwimbaji Ally Chocky kutoka Twanga Pepeta ameongea na Saluti5 na kutoa ufafanuzi juu ya habari za yeye kuanzisha bendi mpya ya kupiga show za ndondo.

Ally Chocky amesema yeye hajaanzisha bendi mpya bali ameanzisha show za Jumatano nje ya bendi yake ya Twanga Pepeta.

Amedai maonyesho hayo ya Jumatano yatajulikana kama “Ally Chocky na usiku wa Mwafrika” na yatakuwa yanafanyika pale tu Twanga Pepeta inapokuwa haina maonyesho kwa siku husika.

Aidha, Chocky amesema kimsingi yeye hajaanzisha bendi mpya, bali atakuwa akikusanya wasanii watakaoimudu program ya maonyesho yake ambayo yatapambwa zaidi na nyimbo za Extra Bongo na chache za Twanga Pepeta na Mchinga Generation.

“Sitakuwa na wasanii wa kudumu, itategemea ni nani yuko huru kwa siku hiyo na nani anaimudu program yangu, najua wako wasanii wengi wanazijua nyimbo zangu, kwahiyo siwezi kupata shida hata kidogo,” alisema Chocky.

“Hii si bendi bali ni show ya Ally Chocky,” aliongeza mwimbaji huyo.

Jumatano usiku Chocky alifanya onyesho lake ndani ya DDC Kariakoo ambapo tangazo lake lilionyesha kuwa atakuwa hapo kila Jumatano.

Hata hivyo Chocky ameaimbia Saluti5 kuwa kwasababu zilizo nje ya uwezo wao, Jumatano ijayo hawatakuwa DDC Kariakoo, bali watakuwa Yombo.


No comments