AMISSI TAMBWE ASEMA KOCHA MASOUD JUMA WA SIMBA HAWEZI "KUIUMBUA" YANGA

MSHAMBULIAJI wa Yanga Amissi Tambwe amesema anamjua vizuri kocha Masoud Juma na kwamba ni kocha mzuri kwa kiwango chake lakini haoni kama anaweza kuiumbua Yanga.

Tambwe amesema kocha Juma anamjua vyema kutoka kwao Burundi lakini ujio wake katika kikosi cha Simba haoni kama anaweza kuzuia mbio za klabu hiyo kuchukua ubingwa.

Tambwe alisema Simba haiwezi kupata mafanikio na Juma na kwamba tatizo kubwa klabu hiyo ni uongozi ambao hata kocha huyo utamshinda  na ataondoka.


Alisema Mburundi mwenzake huyo ni hodari kwa kupandisha morali ya wachezaji kutokana na makeke yake ambayo haoni kama ni kigezo cha kupata mafanikio makubwa.

No comments