ARSENAL KUMPIGA BEI MESUT OZIL MWEZI JANUARI


Arsenal itisikilza ofa za Mesut Ozil mwezi Januari ili kuepuka kumpoteza bure majira ya kiangazi.

Maendeleo hayo yanafungua milango kwa Inter Milan kumnyakua Mjerumani huyo baada ya  Erick Thohir, mtendaji mkuu wa miamba hiyo ya Italia kuweka wazi kuwa timu yake ingependa kuwa na Ozil.

Ozil atabakiza miezi sita tu ya mkataba wake pale dirisha dogo la Januari litakapowadia.

No comments