ARSENAL YAIFANYIA KITU MBAYA EVERTON… kibarua cha Ronald Koeman hatarini


Ni wazi kuwa sasa kocha wa Everton, Ronald Koeman maji yako shingoni na kibarua chake kiko hatarini baada ya kukubali kichapo kizito kutoka kwa Arsenal.

Katika mchezo huo wa Premier League, Everton ikiwa nyumbani ikakubali kulambwa bao 5-2 dhidi ya kikosi cha Arsene Wenger.

Wayne Rooney alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Arsenal kunako dakika ya 12 kabla Nacho Monreal hajasawazisha dakika ya 40 na kufanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa 1-1.

Kipindi cha pili Arsenal ikafunga dakika ya 53, 74 na 90 kupitia kwa Mesut Ozil, Alexandre Lacazette na Aaron Ramsey, huku Baye Oumar Niasse akiifungia Everton bao la pili katika dakika za majeruhi kabla Alexis Sanchez hajaipa Arsenal bao la tano.

No comments