AUDIO: CHRISTIAN BELLA AONGEA MAZITO KUHUSU TANZANIA BAND FESTIVAL
Wakati Christian Bella amekuwa akionekana ni mtu mwenye kujitenga na muziki wa dansi, mwanamuziki huyo ameongea kauli nzito kuhusu muziki wa dansi hususan tamasha lililopewa jina la Tanzania Band Festival.

Akiongea na Saluti5, Bella amesema wazo la Tanzania Band Festival linastahili kuungwa mkono kwa vile ndio njia sahihi ya kuinua tena muziki wa dansi.

Mwimbaji huyo amedai kama tamasha hilo litaheshimiwa na  kuungwa mkono ipasavyo, basi yatapatikana matunda mazuri kwenye muziki wa dansi.

Bella na bendi yake ya Malaika ni miongoni mwa washiriki wa Tanzania Band Festival ambayo inafanyika kwa mwaka wa pili mfululizo.

“Hatujawahi kuwa na tamasha la  bendi, hii ni kama Fiesta ya live band, Q Plus Entertainment na watu wake wanastahili kupongezwa kwa kuanzisha hii kitu,” alisema Bella.

“Kuna weza kuwepo na mapungufu madogo madogo, kuna vitu vya kujifunza. Kama mwakani wakifanya tena hivi wakatapata na wadhamini zaidi, wakongeza mikoa mingine, basi itakuwa kitu kikubwa sana.

“Ni kitu kizuri, inawaweka wasanii karibu. Tukizingatia na tukiwa na heshima, tukiwa na plan nzuri basi tutapata matunda mazuri,” aliongeza Bella.

No comments