Ijumaa ya tarehe 29/10/2017, rapa na mwimbaji nyota wa muziki wa dansi, Msafiri Diouf alifanya ‘interview’ kubwa sana na kituo cha Capital Radio.

Mahojiano hayo yalifanyika live kupitia kipindi cha Lete Raha kinachoruka kila siku za kazi (Jumatatu hadi Ijumaa) kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana ambapo Diouf alikuwa akilambwa maswali na watangazaji Hawa Hassan na Sarah Kipingu.

Katika mengi aliyoongea Diouf, ni maongezi juu ya matumizi ya madawa ya kulevya ndiyo yaliyogusa zaidi hisia za watu.

Diouf ambaye pia alitambulisha wimbo wake mpya “The Bridges”, alizungumzia safari yake ya kutumia madawa ya kulevya na hadi kufanikiwa kwake kuacha madawa ya kulevya.

Sikiliza hapo juu mahojiano hayo ambayo yanatoa funzo kubwa sana kwa jamii.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac