B BAND WALIVYOKAMUA TANZANIA BAND FESTIVAL DODOMA


B Band chini yake Banana Zorro imemaliza ngwe yake katika show ya Tanzania Band Festival mjini Dodoma ndani ya Kisasa Complex.

Hii ni bendi iliyoleta ladha tofauti ambapo ilitesa zaidi katika miondoko ya muziki wa kizazi kipya pamoja na ule wa kunakili kutoka nje nchi ikiwemo “Another Day in Paradise” ya mkongwe Phil Collins, “Show Me The Way” ya Papa Wemba. Hapa pia ilipigwa hadi reggae.

Lakini B Band pia walionyesha kuwa wapo imara hata linapokuja suala la kupiga muziki wa rumba ambapo walitandika nyimbo yao moja ya rumba matata sana.

Ni katika B Band ndipo tupoanza kuona ‘kijiji’ kikinyanyuka na kwenda kucheza, pale walipopiga wimbo wa “Nzela”.
 Mwimbaji Ashura Kitenge 
 Banana Zorro akitesa na sauti yake nzito
 Maneno Uvuruge kwenye solo gitaa
 Nuruel akiimba na Ashura Kitenge
 Banana akiimba na Ashura Kitenge wimbo "Presha"
Hii ndio safu ya waimbaji ya B Band 


No comments