BAADA YA KUTIKISA KAHAMA NA MWANZA, LEO NI TZ BAND FESTIVAL NDANI YA DODOMA


Hakika Tanzania Band Festival imeacha historia katika miji ya Kahama na Mwanza huku leo usiku historia nyingine ikitegemewa kuandika ndani ya Dodoma.

Ijumaa usiku wakazi wa Kahama walilishuhudia tamasha hilo la kipekee ndani ya Uwanja wa Taifa Kahama ambapo idadi kubwa ya mashabiki wa muziki ilijitokeza.

Jana Jumamosi ikawa zamu ya Mwanza, ikatandikwa show ya maana ndani ya Rock City Mall iliyoshuhudiwa na umati mkubwa wa watu.

Leo kuanzia saa 10 jioni hadi usiku mnene, Tanzania Band Festival itaunguruma kwenye kiwanja kipya cha starehe, Kisasa Capetown Complex, Dodoma.

Bendi zitakazoshiriki ni FM Academia, Twanga Pepeta, Msondo Ngoma, Malaika Band na B Band.

No comments