BAO 6 ZATINGA WAVUNI MECHI YA CHELSEA NA ROMA … Qarabag FK 0 - 0 Atletico Madrid


Hii ilikuwa mechi moja matata sana pale magoli sita yalipotinga wavuni kati ya Chelsea na Roma.

Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa kundi C, timu hizo zikatoshana nguvu kwa sare ya 3-3 huku Chelsea ikipoteza uongozi wa 2-1 iliokuwa nao hadi mapumziko kupitia mabao yaliyofungwa na David Luiz dakika ya 11 na Eden Hazard dakika ya 37 wakati lile la Roma likifungwa dakika 40 na Aleksandar Kolarov.

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Edin Dzeko
 Akaisawazishia Roma dakika ya 64 kabla hajaifungia bao la tatu dakika ya 70.

Bao hilo la Dzeko likadumu kwa dakika 5 tu pale Hazard alipoisawazishia Chelsea dakika ya 75.

Katika mchezo mwingine wa kundi C, Qarabag FK na Atletico Madrid zikawana pointi kwa sare tasa.No comments